Moshi.
Umoja wa Makanisa ya Kikristo Mkoa wa Kilimanjaro (CPCT) umeandaa maombi ya siku nne za kuombea ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Askofu mstaafu wa kanisa la T.A.G Jimbo la Kilimanjaro Mashariki, Glorious Shoo ameeleza hayo leo Jumanne Machi 2, 2021 akibainisha kuwa mgeni rasmi atakuwa mhubiri wa kimataifa, Dk Dana Morey ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji na rais wa kampuni ya Morey Coorporation.
"Umoja huu umeamua kuandaa maombi ya siku nne mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuomba toba na rehema kwa mwenyezi Mungu atuepushe na hili gonjwa hatari linalotishia dunia,” amesema Askofu Shoo.
Amebainisha kuwa maombi hayo yanatarajiwa kufanyiwa siku nne kuanzia Machi 11 hadi 14 na kwamba mbali na maombi wafanyabiashara 50 watabadilishana mawazo na Morey.
Mchungaji Ian Tuusime kutoka nchini Kenya amesema Serikali ya Tanzania imechukua tahadhari kubwa katika mapambano dhidi ya corona, sasa viongozi wa dini wana wajibu wa kuendelea na maombi kwa kumshukuru Mungu kwa hatua zilizochukuliwa.
No comments:
Post a Comment