Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi amewataka madiwani na watendaji wa halmashauri ya Jiji la Arusha kuwaelimisha wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya maji ili kuleta manufaa kwa kizaza cha sasa na kijacho.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya kutembelea mradi wa Sh520 bilioni unaotekelezwa jijini Arusha kwa lengo la kumtua mama ndoo ya maji, Kenani amesema viongozi wanatakiwa  kuwaelimisha wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya maji.

Amesema baadhi ya wananchi kuharibu miundombinu ya maji ni kukosa uzalendo kwa nchi yao.

"Kweli mradi huu ukikamilika utagusa kila sekta utakwenda kutatua changamoto za maji na kuwa historia na tuwe mabalozi wa kuelimisha wananchi. Ukiangalia wilaya ya Monduli majirani zetu wamewekewa maji  lakini wameharibu miundombinu  jambo hilo lisijitokeze.

DC KIHONGOSI ATAKA WANANCHI KUELIMISHWA UTUNZAJI MIUNDOMBINU

No comments:

Post a Comment