Kenya

Wanafunzi watatu ambao waliacha shule kwa kukataa kuvalia barakoa kutokana na sababu za kidini, Jumatano wamekamatwa nyumbani kwao katika Kaunti ya Tharaka Nithi nchini Kenya.

Kamanda wa Polisi wa Embu nchini Kenya  Daniel Rukunga ameeleza wanahabari kwamba, wanafunzi hao lazima wakabiliwe kisheria

Wanafunzi hao wawili wa kike wa kidato cha pili katika Shule ya upili ya Turima na mwingine wa kidato cha tatu shuleni Kajiampau, ni wa dhehebu la Kabonokia ambalo linawakataza waumini wake kuvalia barakoa.

Walikamatwa pamoja na wazazi wao kisha wakapelekwa katika kituo cha polisi cha Marimanti.

Naibu Chifu wa Lokesheni ya Ibote, Mauki Mutegi alifichua kuwa wote watashtakiwa kortini.

Bw Mauki alisema wanafunzi hao hawakurejea shuleni mwezi uliopita na walipogundua wanasakwa, walienda mafichoni.

“Wasichana hao walieleza walimu kwamba, kuvalia barakoa ni dhambi na corona inalenga tu watenda dhambi,” akasema Bw Mauki.

Waumini wa Kabonokia mara kwa mara wamegongana na serikali kuhusu elimu ya watoto wao. Wamekuwa wakidai elimu ya shule duniani inaenda kinyume na mafunzo ya dhehebu lao.

SIKIA HII KUTOKA KENYA DINI KABONOKIA WANASEMA KUVALIA BARAKOA NI DHAMBI NA CORONA INALENGA WATENDA DHAMBI TU

Kenya

Wanafunzi watatu ambao waliacha shule kwa kukataa kuvalia barakoa kutokana na sababu za kidini, Jumatano wamekamatwa nyumbani kwao katika Kaunti ya Tharaka Nithi nchini Kenya.

Kamanda wa Polisi wa Embu nchini Kenya  Daniel Rukunga ameeleza wanahabari kwamba, wanafunzi hao lazima wakabiliwe kisheria

Wanafunzi hao wawili wa kike wa kidato cha pili katika Shule ya upili ya Turima na mwingine wa kidato cha tatu shuleni Kajiampau, ni wa dhehebu la Kabonokia ambalo linawakataza waumini wake kuvalia barakoa.

Walikamatwa pamoja na wazazi wao kisha wakapelekwa katika kituo cha polisi cha Marimanti.

Naibu Chifu wa Lokesheni ya Ibote, Mauki Mutegi alifichua kuwa wote watashtakiwa kortini.

Bw Mauki alisema wanafunzi hao hawakurejea shuleni mwezi uliopita na walipogundua wanasakwa, walienda mafichoni.

“Wasichana hao walieleza walimu kwamba, kuvalia barakoa ni dhambi na corona inalenga tu watenda dhambi,” akasema Bw Mauki.

Waumini wa Kabonokia mara kwa mara wamegongana na serikali kuhusu elimu ya watoto wao. Wamekuwa wakidai elimu ya shule duniani inaenda kinyume na mafunzo ya dhehebu lao.

No comments:

Post a Comment