Arusha
Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Nchini Tanzania Bahati Bukuku Amesema Sababu Ya Kuanza Kutoa Wimbo Wa Mwalimu Wa Ndoa Badala Ya Kutoa Movie Ya Mwalimu Wa Ndoa Kama Ilivyo Kuwa Hapo Awali Ni Kuelimisha Jamii Kuhusu Ndoa Na Mungu.
Akizungumza Katika Kipindi Cha Praise Time kinacho Sikika saa 01Pm-04Pm Habari Maalum FM 97.7 Na Mtangazaji Wa Kipindi Hicho Method Charles Amesema Malengo Ya Kuachilia Movie Ya Mwalimu Wa Ndoa Bado Yapo Licha Ya Kuwa Kwa Sasa Ameamua Kuachilia Wimbo Ambao Unaitwa Mwalimu Wa Ndoa.
Aidha Amesema Dhumuni Kubwa La Kuachilia Wimbo Huo Kuwa Wa Kwanza Badala Ya Movie Ambayo Itapatikana Katika Mfumo Wa Dvd Na Platform Mbalimbali za Mitandao ya Kijamii Ni Kwaajili Ya Kukumbusha Watu Kuwa Ndoa Bila Yesu Ni Kitu Ambacho Hakiwezekani.
Amebainisha Kuwa Movie Ya Mwalimu Wa Ndoa Ipo Katika Hatua Za Mwisho Kuanza Kusambazwa Katika Platform Mbalimbali Ili Kuwafikia Watanzania.
Bahati Bukuku Kwa Sasa Anamiliki Ukumbi Wa Maombi Ambao Unapatika Mkoani Daresalaam Lakini Pia Ni Mwimbaji Wa Nyimbo Za Injili Nchini Tanzania akifanya Vizuri na nyimbo kama Waraka wa Hamani, Dunia Haina Huruma , Umewazidi wote na Nyingine Nyingi.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Bahati Bukuku
Huduma : Mwimbaji
Mahali : Daresalaam
No comments:
Post a Comment