Mwimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando mzaliwa wa Tanzania amefichua kwamba hajawahi kuolewa ila ana watoto watatu. 

Akizungumza katika kipindi cha Zinga la Asubuhi cha Radio Taifa mwanamuziki huyo alisema angependa kuolewa lakini atakayemchumbia lazima ajue kwamba yeye amebeba madhabahu ya Mungu. 

 “Lazima ajue kwamba sisi ‘outing’ yetu itakuwa kwenda kanisani, tutakuwa tukifunga na kuomba na wala sio kuonekana tu kwa watu kama wanandoa.” Alisema Muhando. 

 Watoto wake anasema aliwapata mitaani alipokuwa akihangaika mitaani baada ya kutimuliwa nyumbani na ndugu zake wakubwa kwa kubadili dini lakini hakutaka kusema mengi kuhusu watoto hao kwani alipitia mateso akiwa nao. 

 Kulingana naye, waliokuwa wakimsimamia kama msanii wa nyimbo za injili walimtesa sana wakitaka hela kutoka kwake na wengine wakitaka atende dhambi. 

 “Nilipigwa, nilichomwa mwili, yaani ni kama vile yatima anavyofanyiwa na mama wa kambo.” alisema Rose. Mwanadada huyo alisema watesi wake walimzidi kwani wana uwezo mkubwa nchini Tanzania. 

 “Niseme ukweli, Tangu Rais Magufuli kuingia uongozini nimepata amani na ndio unaona nimepona nimerejelea huduma ya uimbaji na hata mwili umenawiri.” alisema Rose ila hakufichua ikiwa aliwahi kukutana na Rais huyo na akapata usaidizi. 

 Kuhusu uzinduzi wa albamu yake ambao umesababisha minong’ono kwenye mitandao ya kijamii, Rose alisema kwamba anatimiza tu alichoagizwa na Mungu. Anadhamiria kujenga kanisa kutokana na hela ambazo atachangisha kupitia kwa uzinduzi wa nyimbo zake mpya. 

 Kiingilio cha halfla hiyo ya tarehe 27 mwezi Februari mwaka 2021 ni shilingi elfu 50 pesa za Kenya na anaomba tu kwamba Rais Uhuru Kenyatta ahudhurie. 

CHANZO CHA HABARI

Mwimbaji: Rose Muhando

Contact :@rosemuhando

Mahali :Tanzania 

ROSE MUHANDO : ATAKAYE NIOA AJUE MIMI NI MADHABAHU

No comments:

Post a Comment