Waumini wa Dini ya Kikristo wametakiwa kuachana na Roho ya Hofu hasa wakati huu ambapo Dunia ipo katika Mtikisko wa Ugonjwa wa Corona.
Hayo yamesemwa na Mchungaji Albert Sindondwa Wakati akihubiri katika Ibada ya Jumapili Kanisa la EAGT Gethsemane Monduli Mkoani Arusha.
Amesma kuwa kwa Nyakati hizi watu walio okoka nao wamekuwa na Hofu kubwa kwa sababu ya Ugonjwa wa Corona badala ya Kujenga Imani kwa Mungu.
Akisisitiza Kuhusu Imani amesema Elisha aliambatana na Elia kwa sehemu kubwa kipindi Elia anakwenda Yeriko na Yordani na wakati huo kulikuwa kunamapito Makubwa lakini kwa Imani Elisha aliongezewa Maradufu.
Aidha Baadhi ya washirika katika Kanisa hilo la EAGT Gethsemane Monduli wamesema wameimarishwa Kiimani katika Ujumbe wa huo na Kuhuishwa Upya kiimani na Kuahidi kuendelea Kusimama na Mungu katika Janga hili la Dunia.
Hata hivyo amesema kuwa Kanisa ni chumvi ya Dunia hivyo linatakiwa kusimamama imara katika Imani katika wakati huu ambapo Dunia ipo katika wakati wa Mpito badala ya Kuingiza Hofu.
CHANZO CHA HABARI
MChungaji : Albert Sindondwa
Contact : +255755419510
Kanisa : EAGT MONDULI
No comments:
Post a Comment