Jamii ya Wakristo nchini Tanzania Imetakiwa Kutambua Nyakati zilizopo na Kuchukua Hatua badala ya Kuendelea Kujenga Hofu na Kuwa na Kupungukiwa na Imani.
Hayo yamesemwa na Bishop Dkt Julius Laizer katika Ibada ya Jumapili iliyo fanyika Katika Kanisa la Naivera Apostolic Church lililopo Ungalimited Mkoani Arusha.
Bishop Dkt. Laizer amesema Faida ya Kujua Majira na Nyakati Inamsaidia Mkristo wa Leo Kujua Jinsi ya Kuisha Maisha ya leo na Kitu gani ambacho anatakiwa Kufanya kwa wakati husika.
“Kujua Majira na Nyakati inasaidia kuweka Mipango na Maamuzi Kitu gani uanze na Kitu gani Ukiache kwa Muda Gani”Alisema Bishop Dkt Julius Laizer.
Amesema Kuwa Wakristo wengi wa Leo wameshindwa kufahamu Majira na Nyakatika na Kupambanua nini wanatakiwa Kukifanya katika Jamii na kufahamu ni Kitu gani kinahitajika Katika jamii Husika.
“Kujua Alama na Nyakati hutusaidia Kujua Mungu amekusudia nini kifanyike kwa wakati huo Kwani Mungu anaweza kutuma Ujumbe wa unyakuo kupitia watumishi wake bila Kujua” Alibainisha Bishop Dkt. Laizer.
Aidha amebainisha Kuwa kujua Majira na Nyakati Humsaidia Mkristo kuwa Mshindi wa Vita ya Kiroho kwa sababu ya Uongozi wa Roho.
Aidha Amesema kuwa Nyakati zilizopo sasa ni Nyakati za Mwisho kwani alama Moja Wapo ni alama ya Kufa Mtu Mmoja moja kufa Vikundi na Unyakuo na Ukiangalia Hivi sasa Vifo vya Mtu mmoja mmojavimeongezeka na Hii inadhihilisha ni Siku za Mwisho.
Aidha kwa sababu ya kuibuka kwa Ugojwa Huu wa Corona amewataka watu Kuokoka na Watakatifu kuendelea Kujitakasa Zaidi kwani siku za Mwisho tayari zimejidhihirisha hasa Kwa wakati huu tuliopo.
Pia Amesema kuwa Mungu sio kuwa hajui kuhusu Covid 19 anafahamu na anasikia Maombi ni vyema Wakristo wakaendelea Kuomba Zaidi.
Nao Baadhi ya Washirika wa Kanisa Hilo akiwemo Blessing Fabiani na Clizanty Mathayo wamesema Kuwa Wamepokea Ujumbe Huo na wataendelea Kujiimarisha Kiimani huku wakitubu na Kujitakasa Kwa Mungu na Kuliombea Taifa la Tanzania na Dunia kwa Ujumla katika Janga Hili la Corona.
CHANZO CHA HABARI
Mchhungaji : Bishop Dkt.Julius Laizer
Contact : +255754386865
Kanisa : Naivera Church Apostolic
No comments:
Post a Comment