Na Method Charles
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili anayemiliki Nyimbo Nane Tangu ameanza kuimba Muziki wa Injili nchini Tanzania Upendo Shayo amesema Waimbaji wa Muziki wa Injili wanao anzisha Makanisa wanatakiwa kuyasimamia Kikamilifu Badala ya Kufuata Mkumbo.
Upendo Shayo ambaye mbali na Uimabji wa Muziki wa Injili Kitaaluma ni Mwalimu wa Masomo yote Isipokua Hisabati katika Shule za Msingi amesema Kama Kweli wameitwa na Mungu haoni Shida lakini kama ni Maamuzi yao Mungu aingilie Kati.
Upendo alisema Hayo Baada ya Kuulizwa na Method Charles katika Kipindi cha Top Ten ya Habaari Maalum Fm 97.7 ambaye Alitaka Kujua Maoni yake kufutia Waimbaji wakongwe Kufungua Makanisa.
Waimbaji ambao wamefungua Makanisa Mpaka sasa ni Christina Shushu kanisa la Dreamer Center, Bahati Bukuku ambaye yeye amefungua Kituo cha Maombi na Maombezi, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) kanisa la Free To worship Church.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Upendo Shayo katika Picha
Upendo Shayo ni Moja ya waimbaji wa Muziki wa Injili ambaye ameamua Kusimama kama Solo Artist Kuanzia Mwaka Jana Mwezi wa Tisa licha ya Kuwa linapo kuja suala la Kuimba ameanza kuimba Tangu akiwa shule ya Msingi.
Shayo kwa sasa anafanya Vizuri na wimbo Wake Mpya Nimesamehewa ambao Unafanya Vema katika Vituo Mbalimbali vya Radio nchini Tanzania ikiwemo Habari Maalum fm 97.7 lakini pia Unapatikana kupitia Youtube Chanel yake inayoitwa Upendo Shayo.
CHANZO CHA HABARI
Mwimbaji : Upendo Shayo
Contact : +255752680658
Kanisa analo Abudu : Kanisa Katoriki Burka
No comments:
Post a Comment