Na Method Charles
Wakristo wametakiwa kufanya kazi Kwa bidii badala ya Kuwekeza katika Maombi Pekee na Kuendekeza uvivu kwa kuamini katika Maombi.
Hayo yamesemwa katika Kanisa la EAGT Mererani linalo simamiwa na Kuongozwa na Mchungaj Frank Msuya Wakati akihubiri katika Ibada ya Jumapili.
Mchungaji Msuya Amesema watu wengi wamewekeza Muda wao Mwingi katika Kuomba na Kuombewa ili kufanikiwa wakiamini kuwa watafanikiwa badala ya Kubuni na kufanya kazi ili kuimarisha Uchumi wa Familia Zao.
Ametanabaisha Kuwa Kuamini Katika Maombi na Kuombewa bila Kufanya Kazi ni Dhambi ikizingatiwa wakati huu ambapo kumekuwa na Vituo vingi vya Maombezi ambapo watu wamekuwa wakishinda wakiomba na kuombewa badala ya Kufanya kazi .
“Unakuta Mtu anashinda kanisani kila siku anaomba badala ya kutenga Muda wa kuomba na Kufanya Kazi Ukisoma Kitabu cha Mithali 10:24” alisema Mchungaji Msuya.
Aidha ameeleza Kuwa Roho ya Mafanikiwa Inatakiwa kuwekezwa Zaidi katika kutafuta kwa Kufanya Kazi Badala ya Kuomba na Kushinda Kanisani.
Pia amesema kuwa Baraka zinafuata na hazifuatwi na zipo kwa pande zote kwa Mwanamke na Mwanaume kila Mtu anaweza kuwa na Mfanikiwa na Baraka Kama atawekeza katika kufanya kazi na Kuomba bila kuwa Tegemezi.
“Sisemi Kuwa watu wasiombe wala Kuombewa ila watenge Muda Mzuri kwaajili ya Kufanya Kazi tena Kwa Bidii na Kuomba na Kuombewa”Alisema Mchungaji Msuya.
Hata Hivyo ameeleza kuwa watu walio Okoka Wana uwezo Mkubwa wa kung’amua Mambo mbalimbali na Kufanya Makubwa kwa sababu ya Kuwasiliana na Mungu kwa Karibu Mara kwa Mara lakini wamekuwa hawayafanyii Kazi yale ambayo wamekuwa wakipewa na kuelekezwa na Mungu ikiwemo ya siri ya Kubarikiwa na Mafanikio
CHANZO CHA HABARI
MChungaji : Frank Msuya
Contact : +255763990033
Kanisa : EAGT Mererani
No comments:
Post a Comment