Na Method Charles
Arusha
KANISA la The Gate of Heaven Centre (GHC) lililopo Maji ya Chai Mkoani Arusha limetoa msaada kwa watoto wanao ishi Mazingira Magumu wa kituo Cha Kalama Kids kilichopo Maeneo ya Balaa.
Akizungumza mara baada ya Kutoa Msaada Huo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa Hilo la The GHC Mch. Zinzendorf David amesema Kanisa hilo limekuwa na Mpango wa kusheherekea na Watoto wanao ishi katika Mazingira Magumu kila mwaka kwa kutoa msaada huo.
Kanisa hilo limetoa msaada wa vifaa vya shuleni kama madaftari, kalamu na Sabauni kwa watoto 12 wenye uhitaji ikiwa ni maandalizi ya masomo watakayoanza Januari 2021.
Izack chikwaze ni Mkurugenzi wa Kituo cha Karama Kids ameshukuru kwa kile ambacho kimepatika katika kanisa hilo na Kubainisha kuwa Mahitaji Makubwa ni mahitaji ya Shule.
Baadhi ya Watoto hao waliofika na Kuhudhulia katika Ibada ya Krismasi wamefurahishwa kwa kupokea Msaada huo na Kuahidi wata utumia Vizuri katika Mahitaji yao ya Kila Siku.
CHANZO CHA HABARI
KANISA LA GHC
CONTACT
+255752210226
No comments:
Post a Comment