Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Jiji lenye sifa ya kipekee katika Kumsifu Mungu nchini Tanzania Arusha aitwaye Elia Sethi amesema alisha wahi kuanua Nguo za Watu ili kupata nguo za Kuvaa Juma pili na baadae kuzirudisha.
Mwimbaji huyo wa Nyimbo za Injili anaye Tamba na wimbo wake wa Nashukuru Mungu amesema hayo Katika Kipindi cha Gospel Climax kinacho Rushwa kupitia Youtube Chanel ya Habari Maalum Media kupitia Link hii Bofya hapa https://bit.ly/3bYcGki.
Sethi amesema alikuwa anafanya matukio hayo sio kwa ubaya kwani alikuwa anatamani kumtumikia Mungu kupitia njia ya Uimbaji lakini hakuwa na Mavazi wala Fedha za Kununulia Mavazi hivyo aliona njia pekee ni kuanua mavazi ya Majira usiku kasha kuyatumia asubuhi na kuyarejesha.
“Kuna siku niliwahi kukamatwa na Mwenye Nguo Kanisani lakini nilimuueleza hali yangu akawa amenielewa na kuniachia Maazi yake licha ya kutaka Kumrudishia alikataa” Alisema Mwimbaji Elia Sethi.
Aidha amesema kuwa Huduma yake ya Uimabji ameanza kuimba Tangu Mwaka 2011 na ana miaka tia katika huduma yake ya uimbaji mpaka sasa.
Katika ushuhuda huo pia Mwimbaji huyo amebainisha kuwa ilimbidi Muda mwimngine awe analala Mlimani ili kutafuta Uso wa Mungu ndipo Mungu alipo Muinua na Kumfikisha hapa alipo Kihuduma.
Sambamba na Hayo amewashukuru watumishi Mbalimnali ambao wamekuwa Msaada katika kuinuka kwake akiwemo Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Peter Mwabulambo na Mtumishi wa Mungu Joe Aminiel ambao wamekuwa msaada kwake.
Hata hivyo amebainisha kuwa kwa sasa anaendelea kumtumikia Mungu katika kanisa la Malango ya Ushindi kama Mwimbaji na Mtu wa kuombea watu ndani ya Kanisa akiwa amesimama katika wokovu mbali na uimbaji anafanya kazi na ameoa ana watoto wawili Mapacha anamshukuru sana Mungu kwa alipo Mtoa.
CHANZO CHA HABARI
Mwimbaji : Elia Sethi
Contact : +255766444655
+255659701521
No comments:
Post a Comment