Wakristo nchini wametakiwa kutenda Mema badala ya kujikita Zaidi katika Maombi na Kushiriki Ibada za Jumapili na Katika ya wiki.
Hao yamesemwa na Mchungaji Kiongozi wa kanisa la FPCT Hai Mkoani Kilimanjaro katika Ibada ya Jumapili ambayo iliongozwa na Mchungaji Cleopa Kweka.
Mchungaji Kweka amehubiri katika kutenda mema nyakati hizi za mwisho huku akisisitiza kuwa ni njia ya kuzaa matunda mema yanayo dumu.
Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki cha nyakati za mwisho
adui amekuwa akiondoa hali ya kutenda
mema na amekuwa akileta na kuondoa hali ya watu wa Mungu kuzaa matunda mema
yanayo dumu kwa Mungu.
Baadhi ya waumini wameeleza kufaidika na mafundisho hayo na kwamba wanatakiwa kutenda mema kokote wanapo kuwa ili kuzaa matunda yanayo dumu kwa Mungu.
Hata hivyo wamebainisha kuwa kunafaida katika kuzaa matunda yanayo dumu katika nyakati hizi za mwisho na kujiwekea hazina mbinguni.
No comments:
Post a Comment