Kocha Yanga Ampa Shavu Carlinhos

 

 

 

KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi kuu.

 

Carlinhos ambaye amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti.

No comments:

Post a Comment