Mwanamziki maaraufu wa nchini Kenya, Rosemary Wahu Kagwi maarufu kwa
jina la ‘Wahuu’ alitangaza kuingia kwenye muziki wa injili mwaka mmoja
uliopita na kuachana na muziki wa kidunia.
Wahuu amesema kuwa hajuti kufanya aina hiyo ya muziki akiwa na
promoti wimbo wake mpya wa ‘Nifanane Nawe’ ambapo ameweka wazi kuhusu
safari yake ya kwenye muziki wa injili
Aidha amesema kuwa anafuraha kubwa kwa mapokezi na kumekuwa na
mrejesho chanya tangu atangaze kuwa anaingia kwenye muziki wa injili.
“Nimepokea nguvu kubwa kutoka kanisani na wanamziki wa injili hivyo
najisika vizuri kwani hata wasnii wasio wa injili pia wananipa
nguvu,”amesema Wahuu
Akizungumzia kuhusu kuwahi kufanya muziki wa kidunia amesema kuwa hajutii kwa sababu ilikuwa moja ya sehemu ya safari yake.
No comments:
Post a Comment