
Kuna
video imesambaa ikimuonyesha Mwimbaji Mkongwe wa nyimbo za Gospel Rose
Muhando akifanyiwa maombi ambapo kila mmoja amekuwa na maoni yake baada
ya kuitazama. Hapo chini ni mtazamo wa Msanii wa Injili, Emmanuel
Mbasha.
'Nikiwa
kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili
Tanzania, napenda kuweka wazi kuwa nimehuzunishwa sana na hii video ya
maombezi ya muimbaji mwenzetu Rose Muhando.
Kwa
unyenyekevu kabisa naweza kusema kuwa, maombi ni muhimu sana kwa watu
wote, ila namna ya kuombea ikiwa mbaya inaweza kuharibu umuhimu wote wa
maombi na kusababisha maombi yadharaurike au yamdharaulishe aliyeombewa.
Katika
nia yangu ya ndani nimefurahishwa sana na kitendo cha Rose kuombewa,
ila kero yangu kubwa imekuwa kwenye njia iliyotumika kumuombea. Rose
Muhando ni star, na katika medani za mziki wa injili ni mtu anaetazamwa
na watu wengi sana kama rol model wao, hivyo nadhani ilikuwa ni bora
zaidi kuwa waangalifu katika kumuombea ili kulinda brand yake.
Biblia
inasema, mwenye heshima apewe heshima, hivyo kwangu mimi sidhani kama
mchungaji aliyemuombea Rose amempatia heshima anayostahili, maana
binafsi sikuona haja ya kuwasha camera na kuanza kumuombea hadharani
vile.
Hali
hii inaweza kumtangaza sana muombeaji lakini kwa upande wa muombeaji
inaweza kuzidisha tatizo na kusababisha adharaulike zaidi kwenye jamii
inayomtazama. Watumishi wa Mungu mahitaji kuwa na hekima pamoja na kifua
cha kutunza siri, na siyo kufanya mambo kwa mihemko huku mkitazama
maslahi yenu.
Mimi
nadhani ingekuwa bora sana endapo mchungaji angemuombea ofisini, na
kama maombi yangeleta majibu naamini video ya shuhuda ambayo Rose
Muhando ange ongea wakati akiwa na akili zake timamu ndiyo ingefaa
kusambaa na kuendelea kumjengea heshima yeye pamoja na mtumishi
aliyemuhudumia.
Kumbuka
yule Akida (mkuu wa vikosi cha askari wa kirumi) alipohitaji maombi kwa
Yesu, Biblia inasema Yesu alifunga safari kwenda nyumbani kwake ili
kumuombea. Unadhani kwanini hakumwambia apelekwe amuombee hadharani kama
alivyofanya kwa Batromayo? Hii ilikuwa ni hekima ya kulinda heshima ya
muombewaji. Maana huwezi kumuombea Rais kama unavyoombea ombaomba au
mpiga debe.
Kwa
kweli nimeamua kuwa muwazi na kuziweka huzuni zangu hadharani ili
waombeaji mjirekebishe. Siyo kila maombi yafanyike wakati caméra ziko
on, kuna mengine ya kuzima camera na kuomba kwa staha ili kuendeleza
uhai na kipawa'
No comments:
Post a Comment