Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia imepiga marufuku walimu wa shule za msingi na sekondari kutembea na viboko kwenye maeneo yao ya shule pamoja na kuwataka kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utoaji wa adhabu za viboko kwa wanafunzi kulingana na waraka wa elimu wa mwaka 2002 unavyoelekeza.

Agizo hilo limetolewa na naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia William Ole Nasha wakati akifungua mafunzo kuhusu uimarishaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa walimu wa ziada 443 wanaofundisha darasa la kwanza na la pili kutoka halmashauri sita za mikoa ya Mwanza na Kagera, ikiwa ni siku chache baada ya kifo cha mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Kibeta manispaa ya Bukoba Sperius Eradius baada ya kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wake wa nidhamu.

Mtendaji mkuu wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu ADEM Dkt. Siston Masanja Mgullah amesema adhima ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kuendelea kuwapatia walimu wengi mafunzo ya ufundishaji wa stadi za KKK pamoja na mbinu zingine za ufundishaji ili kuwa na walimu bora kwa elimu bora.

Mafunzo hayo katika kituo cha chuo cha ualimu Butimba yatawahusisha zaidi ya walimu 900 katika awamu mbili.

Serikali yapiga marufuku walimu kutembea na viboko

No comments:

Post a Comment