Na Jusline Marck
Rais wa mtandao wa wasanii wa injili Tanzania TAGOANE Dkt.
Godwin Maimu Nyaka amewataka waimbaji wa nyimbo za injili kujiwekea akiba
ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuwawezesha kumuhubiri Mungu.
Dkt. Nyaka ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi DVD ya muimbaji wa nyimbo za injili Magreth Laizer
iliyofahamika kwa jina la UHIMIDIWE ambapo ameeleza kuwa bado waimbaji wengi wa
nyimbo za injili wanaishi maisha ya kuungaunga kutokana na kipato kidogo
walichonacho.
Aidha amesema kuwa kupitia TAGOANE watahakikisha wanaisajili
kazi ya muimbaji hiyo katika baraza la taifa.
Kwa upande wake Magreth Laizer mwimbaji wa nyimbo za injili
wa kujitegemea kutoka katika kanisa la KKKT Ushirika wa Suye amesema kuwa lengo
la uzinduzi huo ni kupata fedha zitakazo muwezesha kusonga mbele katika huduma
ya uimbaji.
No comments:
Post a Comment