Band ya Muziki wa injili nchini Tanzania New Life Band
imeadhinisha miaka 40.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Band hiyo Dr Ondo ambaye pia ni
mwanzilishi amesema tangu kuanziashwa
kwa bend hiyo kumeleta mabadiliko makubwa kwa vijana wengi hapa nchini.
Dr Ondo amesema kwa
sehemu kubwa wameweza kubadilisha maisha ya vijana kupitia kambi za mafunzo ya neno la Mungu
ambazo zilikuwa zikifanyika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Aidha Dr Ondo ameishukuru Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kuwapa uhuru wakuendelea kutoa huduma ya uimbaji na mafunzo ya
neno la Mungu kupitia kambi mbalimbali
ambazo zimekuwa zikiendeshwa hapa nchini kwa miaka (25)sasa.
Hatahivyo Dr Ondo ameongeza kuwa miongoni mwa huduma zao pia
wamefanikiwa kufungua shule ya New Life Secondary iliyopo monduli kwa miaka (10)iliyopita.
Ikumbukwe kuwa New life ndiyo bend ya kwanza ya uimbaji
nyimbo za injili kuanzishwa hapa nchini tangu mwaka wa 1978 na chanzo cha
kuanzishwa kwa bendi nyingine za muziki wa injili.
No comments:
Post a Comment