Mchungaji wa kanisa la Grace and Power Prophetic Ministry
International huko nchini Nigeria, David Elijah amenusurika kifo baada
ya kushambuliwa kwa risasi akiwa njiani kuelekea kanisani.
Mchungaji Elijah ni miongoni mwa wachungaji vijana na tajiri nchini Nigeria.
Ijumaa ya Septemba 7, 2018 akiwa mjini Awka, Anambra huko Nigeria
kwenye gari yake akielekea kanisani kwake alivamiwa na majambazi
waliokuwa na silaha za moto na kuanza kumfyatulia risasi.
Nusu ya gari hilo lilitobolewa kwa risasi maaskari walifika eneo la
tukio na kumkuta mchungaji David Fulana yake ikiwa yenye matundu ya
risasi huku mwili wake ukiwa haujajeruhiwa hata kidogo.
Hata hivyo, maaskari hao walimkamata kwa mahojiano zaidi huku
wakitahamaki tukio hilo kwamba amewezaje kupona kwenye shambulizi hilo.
Tayari Jeshi la Polisi katika jimbo la Anambra limemuachia Mchungaji
huyo siku ya Jumamosi baada ya kujiridhisha kuwa mtu huyo alikuwa salama
na ni raia mwema.
Mchungaji David anatajwa kuwa moja ya wachungaji vijana wenye utajiri
Mkubwa nchini Nigeria. Baada ya tukio hilo la kushambuliwa jana David
alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika maburungutu ya
fedha huku akiweka Captions kuwa yupo nchini Malaysia kikazi.
No comments:
Post a Comment