Na Jusline Marck
Wakristo
wametakiwa kuondoa nadhiri ambazo wameziweka mbele ya mungu ili kuweza
kuepukana na dhambi ya udanganyifu.
Akihubiri
kwenye ibada ya jumapili mchungaji kiongozi wa kanisa la kiinjili ya kirutheri
Tanzania dayosisi ya Meru jimbo la Magharibi Usharika wa Patandi Franael
Issanja amesema kuwa dhambi ya udanganyifu ndiyo ilimfanya anania na safira
kufa.
Aidha
amesema kuwa msingi wa mkristo umejengwa ndani ya mkristo ili kumshukuru
mungu kwani moyo wa mwanadamu ni sadaka mbele za mungu.
Katika
ibada hiyo Mch. Franael ameweza kunukuu maandiko kutoka katika kitabu cha
matendo 5:1-11 na kueleza kuwa ni wajibu wa mkristo kumshukuru mungu kila
wakati.
Ibada
hiyo iliongozwa na kichwa kisemacho SHUKURANI ZETU ambapo Mch. Franael
amefafanua kuwa dhambi ya kumdanganya Roho Mtakatifu inamfanya Mungu ajitenge.
No comments:
Post a Comment