Na Uvenal Kimario
Kilimanjaro
Jamii mkoani Kilimanjaro imeshauriwa kuishi maisha ya kumpendeza
Mungu,kuwa na hofu ya Mungu kwa lengo la kuhakikisha Imani yao inakua
kila siku.
Ushauri huko umetolewa na Mchungaji wa kanisa la Efatha
Ministry Kilimanjaro Agape Komba katika ibada ya leo ambapo amesema
endapo jamii itaishi ikimpendeza Mungu itazidisha chachu ya watu kuwa na
nguvu ya Mungu kwa kulinda mioyo yao isichafuke.
Amesema kwa sasa wanadamu waliowengi wamekua wakiishi kwa
mazoea kwa kumzoelea Mungu hali ambayo inasababisha kukosa utii katika
neno LA Mungu.
Katika mahubiri hayo Mchungaji Komba amesisitiza na kutilia
mkazo katika somo la Pokea Maarifa kutoka kitabu cha Mathayo 5:1-14
linalohusu uhalisia was mwanadamu juu ya utii,kuwa na mioyo safi ili
kutimiza mapenzi ya Mungu.
No comments:
Post a Comment