Na Jusline Marck
Arusha
Ili mtu aweze kuwa huru katika Kristo Yesu anapaswa kumjali na kumuonyesha mwingine upendo utokao kwa Baba kwani mkristo ameitwa ili apate uhuru na siyo kwa ajili ya mambo ya mwilini.
Ili mtu aweze kuwa huru katika Kristo Yesu anapaswa kumjali na kumuonyesha mwingine upendo utokao kwa Baba kwani mkristo ameitwa ili apate uhuru na siyo kwa ajili ya mambo ya mwilini.
Akihubiri
katika ibada iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT Jimbo la Magharibi
Usharika wa Patandi lililopo Tengeru Mkoani Arusha Parishi.
Mchungaji wa kanisa
hilo Victoria Stanslaus amesema kuwa watu wengi wapo katika mambo ya
mwilini na kushindwa kufanya ya rohoni.
Aidha amewataka wakristo kuwapenda jirani zao kama nafsi zao nao
watamuona mungu akitenda mambo makuu ambapo amefafanua kuwa Yesu Kristo
alikuja duniani ili kumuweka mwanadamu huru.
Sambamba
na mahubiri hayo ibada hiyo iliambatana na maombezi ambayo yaliongozwa
na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Franael Isangya(isanja)ambapo
amesema kuwa maombi hayo hufanyika kila mwezi jumapili ya tatu kwa lengo
la kuwafanya wakristo kuweza kupokea majibu ya maombi yao.
No comments:
Post a Comment