Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania TAA, kwa kuchukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa wa Ebola
usiingie nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu jijini Dar es salaam katika hotuba yake kwa wananchi
walioshiriki Matembezi ya hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia
ugonjwa huo usiingie nchini.
Ummy Mwalimu amesema TAA
inafanya jambo jema kwa kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini kupitia
viwanja vya ndege wanafanyiwa ukaguzi na kutoa taarifa za afya zao kwa wale
ambao watabainika kuwa na joto la mwili lisilokuwa la kawaida.
Aidha, amesema pamoja na
ugonjwa huo kutoingia nchini, lakini kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la
Afya Duniani WHO, tayari imeripotiwa wananchi 111 wa Kongo wamepata maambukizi
na kati yao 75 sawa na asilimia 67 wamefariki.
Hata hivyo, Ummy Mwalimu
amewaomba Viongozi wa Dini kutumia majukwaa yao katika mahubiri yao kutoa
tahadhari kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa huo wa Ebola.
No comments:
Post a Comment