Huko nchini Marekani Askofu aliyekuwa akiongoza ibada ya
mazishi ya gwiji wa muziki nchini humo, Aretha Franklin amejikuta akishambuliwa
mtandaoni baada ya kuonekana akishika kifua cha Ariana Grande wakati ibada ya
mazishi ikiendelea.
Picha na video zinamuonyesha Askofu Charles H Ellis
wakimshika Ariana juu ya kiuno chake huku vidole vyake vikiwa vimeshikilia
upande mmoja wa kifua chake.
“Sio lengo langu kumshika mwanamke kifua chake”, aliambia shirika
la habari la AP.
Aliongeza, “Pengine nilivuka mpaka, pengine nilijihisi kuwa
karibu naye sana kama rafiki. Lakini tena naomba msamaha.
Muhubiri huyo balisema kuwa aliwakumbatia wasanii wote waume
kwa wake wakati wa shrehe hiyo ya kumuaga malkia wa muziki wa soul.
Lakini waliohudhuria walianza kutuma picha kutoka katika ibada hiyo
wakati Ariana aliposimama na kuanza kuimba wimbo wa Aretha Franklin ‘You
Make Me Feel a natural Woman’.
Watu wengi walihisi kwamba mkono wa Askofu Ellis ulikuwa juu zaidi ya mwili wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokuwa akizungumza naye na kusema kuwa hakupendelea kushikwa hivyo.
Watu wengi walihisi kwamba mkono wa Askofu Ellis ulikuwa juu zaidi ya mwili wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokuwa akizungumza naye na kusema kuwa hakupendelea kushikwa hivyo.
https://twitter.com/monaeltahawy/statushttps://twitter.comhttps://twitter.com/monaeltahawy/status/1035683239912976386/monaeltahawy/status/1035683239912976386https://twitter.com/monaeltahawy/status/1035683239912976386/1035683239912976386
No comments:
Post a Comment