Serikali imemaliza mgogoro wa Kanisa la African Mission Evangelism
Church ( AMEC TANZANIA ) Arusha uliodumu kwa zaidi ya miaka 13.
Kumalizika kwa mgogoro huo kunatokana na viongozi wakuu wa kanisa
hilo waliokuwa kwenye mgogoro kukubaliana kumaliza tofauti zao baada ya
serikali kuamua kuingilia kati kulinusuru kanisa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro amesema mgogoro
huo haukuwa na tija kwa kanisa wala wananchi waliokuwa wakipata Huduma
za kiroho na ulihatarisha amani na usalama kwa waumini wa kanisa.
Pia amesema mahusino mabovu ya serikali na kanisa hilo yamechangia kudhoofisha kanisa hilo Tanzania kwa zaidi ya miaka 13.
DC Muro amewapongeza viongozi wakuu wa kanisa hilo
kwa kukubali kukaa katika Meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao,
ambapo amewataka viongozi hao wakuu kufanya ibada ya pamoja ya toba
ambayo itawahusisha waumini wote wa kanisa hilo.
“Serikali ya Rais John Magufuli itayalinda makubaliano haya
pamoja na kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yenu,”amesema.
No comments:
Post a Comment