Mwita Waitara mbunge aliye
hama kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kwenda CCM
afanyiwa Maombi Kanisani Dar es salaam
Mwita Waitara ni miongoni mwa
Wabunge wawili waliojiunga na CCM hivi karibuni kutokea Vyama vya upinzani na
sasa amechaguliwa na
CCM kugombea tena
Ubunge kwenye Jimbo hilohilo la UKONGA ambalo alikua Mbunge wake kupitia CHADEMA kabla ya kujiunga na CCM.
Wakati huu ambapo anajiandaa
kuingia kwenye Uchaguzi wa marudio, Mwita amehudhuria ibada kwenye Kanisa la WRM Kivule Dar es salaam na
kufanyiwa maombi na kiongozi wa Kanisa hilo Nicolaus Suguye kama inavyoonekana kwenye picha.
No comments:
Post a Comment