Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola
amesema hatasita kufuta makanisa au misikiti inayoshindwa kutatua
migogoro ya taasisi hizo.
Ametoa kauli hiyo leo Julai 29, 2018 katika Kanisa la Pentekoste la Leganga, lililopo Arumeru mkoani Arusha.
“Kuanzia sasa, kanisa lolote au msikiti
wowote utakaokumbwa na migogoro na kushindwa kuitatua wenyewe; misikiti
hiyo, makanisa hayo nitakwenda kuyafuta mara moja,” amesema.
Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha yanakuwapo makanisa na misikiti inayohubiri amani na utulivu.
Waziri Lugola ameonya askari Polisi
wanaowashusha jukwaani masheikh na wachungaji inapofika saa 12:00 jioni,
akisema muda huo ukifika waimarishe ulinzi ili waumini wamalize ibada
zao vizuri.
No comments:
Post a Comment