Polisi katika wilaya ya Pader nchini
Uganda wamemkamata mwanaume mwenye miaka 30 baada ya kumpiga mtoto wake
wa miaka 7 kwa fimbo mpaka kufa kisa tu mtoto huyo amekataa kwenda
shule.
Richard odokonyero mwenye miaka 7
alikuwa akisoma katika shule ya msingi Pader kabla ya uhai wake
kukatishwa na baba yake Denis Omony Juni 6,2018.
Mwenyekiti wa eneo hilo Charles Otto
Lalobo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa baba huyo
aligeuka hayawani na kumshambulia mwanae kwa fimbo kichwani kabla ya
kufariki.
Inadaiwa kuwa mtoto huyo aligoma kwenda
shule kwa kile alichokidai kuwa anatendewa vibaya na mama yake wa kambo
na alikuwa akimuomba baba yake ampeleke kwa bibi yake akaishi huko.
Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi katika
mkoa wa Aswa River Jimmy Patrick Okema amesema kuwa mtuhumiwa huyo
ameshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Pader na atashitakiwa kwa kosa
kuua punde tu upelelezi ukikamilika.
No comments:
Post a Comment