Mhadhiri Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (Udom) Rose Malfred (31), Mkazi Wa
Swaswa Ameuwawa Kwa Kuchonywa Visu Hadi Kufa Sehemu Mbalimbali Za Mwili
Wake Na Mume Wake Mchungaji Wa Kanisa La TAG John Mwaisango.
Akizungumza Na Waamdishi Wa Habari Mganga Mfawidhi Wa Hospitali Ya
Rufaa Ya Mkoa Wa Dodoma Dk. Calorine Damian Alisema Kuwa Mwili Wa
Marehemu Waliupokea Juzi Usiku Majira Ya Saa Tano.
Alisema Kuwa Mwili Huo Ulipokelewa Hospitalini Hapo Kutokea Maeneo Ya
Swaswa Jijini Dodoma Ukiwa Na Majera Mengi Ya Visu Katika Maeneo
Mbalimbali Ya Mwili.
Dk.Damiani Alieleza Kuwa Kutoka Na Marehemu Kuchonywa Na Idadi Nyingi
Ya Visu Mwilini Mwake Ndiko Kulikopelekea Kupoteza Uhai Wake.
“Mwili Ulipokelea Katika Hospitali Yetu Ya Rufaa Ya Mkoa Majira Ya
Saa Tano Usiku Wa Juzi Ukitokea Maeneo Ya Swaswa Lakini Kutokana Na
Kuchomwa Visu Vingi Kwa Kiasi Kikubwa Kulisababisha Atokwe Na Damu
Nyingi Hadi Kupoteza Uhai Wake”Alisema Dk, Damiani.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Gilles Muroto Alithibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Na Kudai Kuwa Bado Wanaendelea Na Uchunguzi.
“Ni Kweli Tukio Hilo Limetokea Bado Tunaendelea Kufanya Uchunguzi Ili
Kuweza Kubaini Chanzo Cha Tukio Harafu Baadae Tutatoa Taarifa Kwa
Vyombo Vya Habari”Alisema Kamanda Muroto.
Alisema Uchunguzi Wa Awali Unaonyesha Kuwa Ni Wivu Wa Mapenzi Ndio
Chanzo Cha Mauaji Ya Muhadhiri Huyo Aliyekuwa Anaishi Eneo La Swaswa
Jiji Hapa.
Taarifa Zinadai Kuwa Mchungaji Huyo Alifanya Tukio Hilo Mnamo Tarehe 25 Mwezi Huu Nyumbani Kwake Jikoni
Kwa Upande Wake Afisa Habari Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (Udom) Betrece
Bartazar, Alisema Kuwa Ni Kweli Wamepokea Tarifa Za Kifo Cha Mtumishi
Wao Na Kudai Kuwa Mambo Mengine Yanayohusina Na Tukio Hilo Waulizwe
Polisi Ndiyo Wenye Majibu Ya Kutosha.
“Kweli Marehemu Alikuwa Ni Muhadhiri Wa Chuo Cha Udom Na Ni Kweli
Amefariki Hayo Ndiyo Ninayo Yafahamu Kwa Maelezo Mengine Ya Ziada
Muwaulize Polisi Ndio Wanalisimamia Suala Hili Kwa Sasa”Alisema
Bartazar.
No comments:
Post a Comment