Waziri ya Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi
Msajili wa vyama vya kijamii, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na
Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba
kufuatia sakata la barua iliyotumwa kwa Baraza la Maaskofu KKKT na
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Dkt. Nchemba amesema kuwa
Serikali imeanza kufanya uchunguzi na endapo watabaini aliyetengeneza
barua hiyo kwa taasisi hizo za kidini watamchukulia hatua kali za
kisheria.
Amesema uamuzi wa kumsimamisha kazi Komba kupisha uchunguzi unatokana
na taharuki iliyosababishwa na barua hiyo isiyokuwa na baraka za
Serikali.
Aidha, amevishangaa vyama vya siasa ambavyo vilianza kutoa matamko na misimamo hata kabla Serikali haijatoa kauli yake.
Jana, Uongozi wa Bunge ulimzuia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kujibu
swali la mbunge wa upinzani kuhusu kilichoandikwa kwenye barua
iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ililolipa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka iliotuoa wakati wa Pasaka.
Spika Ndugai alifikia uamuzi huo kwakuwa swali hilo liligusa suala la
dini ambalo amewahi kuzia lisijadiliwe ndani ya Nyumba hiyo ya
wawakilishi wa wananchi.
No comments:
Post a Comment