Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amewasilisha ombi rasmi ili nchi
hiyo ijiunge tena na Jumuiya ya Madola baada ya kujitoa mwaka 2003,
wakati wa utawala wa Robert Mugabe.
Zimbabwe ambayo ilitawaliwa na Uingereza, ilijitoa kwenye Jumuiya ya
Umoja wa Madola baada ya Mugabe kutupilia mbali ukosoaji wa sera zake za
kuwanyang’anya raia wa kigeni mashamba na kuwagawia wazawa pamoja
ukosoaji mkubwa juu ya mfumo wa uchaguzi. Ukosoaji huo ulikuwa na
shinikizo zaidi kutoka Uingereza.
Katika kuhakikisha uhusiano wa Zimbabwe na Jumuiya ya Madola unarejea
kama ilivyokuwa kabla ya mwaka 2003, Rais Mnangagwa amewakaribisha
waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya hiyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Jenerali Patricia Scotland amesema
kuwa Mnangagwa ambaye alichukua nafasi ya Mugabe Novemba mwaka jana,
aliwasilisha barua hiyo ya maombi Mei 15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment