Pakistan jijini Karachi, vyombo vya habari vimeripoti juu ya vifo vya
watu 65 waliofariki dunia kutokana viwango vya juu vya joto
lililoikumba mji huo katika siku tatu mfulilizo msimu huu wa mfungo wa
ramadhani kwa waislamu.
Ambapo siku ya jumatau kulikuwa na nyuzi joto 44 hali ambayo iliwawia
vigumu hasa waislamu ambao wamefunga kula chakula na kunywa maji
kipindi cha siku.
Karibu miili 114 ilidhurika na joto kali jijini humo na kukimbizwa
katika Taasisi ya kutoa misaada ya kijamii ya Edhi iliyopo Karachi,
ambapo kati yao watu 65 walifariki dunia.
Hata hivyo matukio hayo ya vifo yanaaminika kutokea yakichochewa na
kukatika kwa umeme katika jiji hilo huku sababu nyingine ikitajwa kuwa
wagonjwa hao kuchelewa kupatiwa matibabu ya haraka.
No comments:
Post a Comment