Msanii maarufu wa muziki duniani, Beyonce amenunua jengo la kanisa kongwe mjini New Orleans nchini Marekani.
Kanisa hilo ambalo limejengwa kwa mawe miaka ya 1900’s limemgharimu Beyonce kiasi cha dola $850,000 sawa na tsh bilioni 1.9 za Kitanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mitandao mbalimbali ya burudani duniani ikiwemo TMZ na Shaderoom zinaeleza kuwa lengo la kununua kanisa hilo ni kueneza dini yake ya Beyism.

Beyism ni dini ambayo wafuasi wake wanamsujudu Beyonce kama mungu wao na tayari imeshapata maelfu ya wafuasi nchini Marekani.

Mwaka 2014, waumini wa dini ya Beyism walianzisha kanisa lao rasmi la Beyonce walilolipa jina la ‘The National Church of Bey’ huko mjini Atlanta nchini Marekani.

Waumini wa Kanisa hilo wanaimba nyimbo za Beyonce na kusoma biblia maalumu zinazoitwa beyble.

Kanisa hilo la Beyonce limepambwa na picha nzuri za Beyonce akiwa amevalia mavazi ya nguo kama za viongozi wengine wa makanisa ya kikristo.

Nchini Tanzania baadhi ya wa Mungu akiwemo Mchungaji wa Kanisa la EAGT  Tanzania Mchungaji Frank Msuya amesema mtu yeyote ambaye ni Maarufu  anauwezo wa kushawishi  kitu chochote ambacho ni cha Kimungu na ambacho sio cha Kimungu.

Amesema kwa Kitendo cha Msanii Beyonce kuanzisha  Dini yake  na Kutengeneza Biblia yake ni Roho ya Udanganyifu ambayo imeambatana na maagano ya Kishetani na kwa Mkristu wa sasa anaye ongozwa na Roho wa Bwana lazima atapuuza jambo hilo na kulitupilia mbali.

 “Mtu yeyote anapokuwa maarufu anaweza kufanya chochote  kwa sababu anawatu lakini kiimani  hawawezi kupata chochote pia vitu hivyo vinambatana  na maagano  kwani tayari wamejiunganisha shetan” alisema Mchungaji Msuya Frank.

Hata hivyo kibiblia amesema  watu wa aina hiyo  huwa hawawezi kufika mbali Mungu atabaki kuwa Mungu na Binadamu atabaki kuwa Mwanadamu.

Mwanamuziki wa Nyimbo za Kidunia Anunua Kanisa na Kuanzisha Dini yake

No comments:

Post a Comment