Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la
Mary Miyombo (32), mkazi wa Kata ya Hombolo, Bwawani mkoani Dodoma
amenusurika kufa baada ya kukatwa koromeo na mumewe wake aliyejulikana
kwa jina la Mgowela Anderson.
Chanzo cha kisa hicho kilichotokea Mei
16, mwaka huu kinaelezwa ni wivu wa kimapenzi ambapo inadaiwa mwanamke
huyo alikutwa na mwanamume mwingine ndipo mumewe akamjeruhi kwa kumkata
na panga kwenye koromeo na kukimbia.
Akizungumza kwa tabu huku akilia, Mary
ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
amesema siku ya tukio akiwa ametoka kuuza pombe kilabuni kijijini hapo
alifika nyumbani kwake na kwenda anapoweka fedha zake ambapo aligundua
1,000 haipo jambo lililosababisha kumuuliza mume wake huyo.
“Nilipomuuliza tu kama amechukua hiyo
hela ndipo kipigo kilipoanza hadi kufikia hatua ya kunikata na panga
shingoni, yaani simtaki tena yule mwanamume kwani hii ni mara ya tatu
ananipiga na kunijeruhi na nimekuwa nikimsamehe lakini kwa hili simtaki
tena,” amesema Mary.
Mganga Mfawidhi wa hiyo, Caroline Damian
amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo hospitalini ambaye alilazwa wodi
namba 10 na tayari amesharuhusiwa.
Hata hivyo, Kamanda wa polisi Mkoani Dodoma Gilles Muroto alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana.
No comments:
Post a Comment