Mtu mmoja nchini Uganda anayejulikana kwa jina la Michael Aboneka
amelishtaki kanisa la Watoto Church akipinga kanuni za utaratibu wa
kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.
Aboneka amefungua kesi hiyo katika mahakama ya katiba iliyopo Jjini
Kampala kulishtaki kanisa hilo ambapo baadhi ya waumini wameonyesha
kuunga mkono taratibu hizo na wengine kupinga taratibu hizo.
Amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya
kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka
18 kama katiba ya Uganda inavyosema.
“Kwanza wanasema nilazima upate barua kutoka kwa wazazi wa bibi
harusi ambayo wanaita Baraka. Kwangu inakwenda na kinyume cha katiba
kifungu 31 ya ndoa ya pili ni kukabidhi barua ya Dakitari ya majibu ya
kupima virusi vya ukimwi kwa kanisa,”amesema Aboneka.
Hata hivyo, Michael Aboneka ameongeza kuwa siyo kanisa la watoto
pekee lenye utaratibu huo bali makanisa mengi nchini humo yanafanya
hivyo na anasema ameiomba mahakama ya katiba kuanza mara moja
kusimamisha kanuni hizo na anatarajia wiki hii mahakama inaweza kutoa
jibu.
No comments:
Post a Comment