Hadi sasa watu 25 wamepoteza
maisha na 54 kuambukizwa, huku wengine 1,139 wakiChunguzwa kwa karibu
baada ya kukaribiana na watu waliambukizwa.
Kauli hii imetolewa na Askofu wa Kanisa hilo Fridolin Ambongo ambaye
ametembelea mji wa Mbandaka na Bikoro maeneo ambayo yameathiriwa na
ugonjwa huo.
Askofu Ambongo amesema, hofu imetenda kote katika maeneo
yaliyoathiriwa na Kanisa Katoliki, limesitisha kwa muda mikutano ya
hadhara ikiwepo, ubatizo na ibada ya kuwasimika makasisi iliyokuwa
imepangwa kufanyika tarehe 3 mwezi ujao katika mji wa Mbandaka,
imeahirishwa.
Kanisa hilo, limeungana na maafisa wa afya kutoa wito kwa wakaazi wa
Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, kuacha kusaliamiana au hata kugusana
na kunawa mikono yao kwa sabuni na maji safi, ili kuepuka kuambukizwa
ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani WHO, nalo limeedelea kutoa chanjo katika njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa huu hatari.
No comments:
Post a Comment