Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa
itayatengeneza na kuyauza magari yaliyorundikwa katika vituo vya Polisi
ili kupunguza msongamano wa magari mabovu vituo humo.
Hayo yamebainishwa na Wizara hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati
akijibu swali la Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa(CCM), Ritta Kabati
aliyehoji, Katika mkoa weti wa Iringa Kuna magari ambayo yanaharibika
tu kidogo yanawekwa katika vituo, unakuta sasa kuna mrundikano mkubwa wa
magari mabovu sasa ni kwanini sasa serikali either au iyauze haraka
sana ili yaweze kusaidia upungufu uliopo katika Mkoa wa Iringa?
“Niseme tu sisi kama serikali tunapokea ushauri huo tutayatengeneza
yale yanayo yanatengenezeka na tutafanya utaratibu wa kuyauza yasiyoweza
kutengenezeka,” amesema Mwigulu.
“Kwa upande wa pikipiki nilishatoa mapendekezo vijana hawa wa
bodaboda wanaokamatwa kwa makosa madogo madogo wafanye utaratibu wa
kuandikisha na kurudishiwa pikipiki zao na waweze kulipia kama kuna
faini walikuwa wanatakiwa kulipa kuliko kuzirundika pikipiki hizo na
kuendelea kuharibika.”
No comments:
Post a Comment