ZAIDI
ya watoto wa kike 28,000 wenye umri wa miaka 14 wanatarajiwa kupatiwa
chanzo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Ruvuma.
Watoto hao ambao wanakadiriwa kuwa 28,676 wanatoka katika wilaya na halmashauri zote za mkoa huo huku wadau na vyombo vya habari wakiombwa kuhamasisha kampeni hiyo ili iwe na mafanikio.
Akizungumza jana katika mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa kwa waandishi wa habari kuhusiana na chanjo hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Gozibert Mutahyabarwa, alisema vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika kufikisha ujumbe huo kwa jamii ili kuwaokoa watoto wa kike na hatari hiyo ya kukumbwa na saratani hiyo kwa kukosa chanjo.
Dk. Mutahyabarwa alisema chanjo hiyo itaendelea kutolewa kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma za afya ya mama na mtoto zikiwamo hospitali, vituo vya afya na zahanati na sehemu zitakazotolewa huduma tembezi hasusan shuleni.
Dk. Mutahayabarwa alizitaja dalili za saratani ya mlango wa kizazi kuwa kutokwa na damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana, maumivu ya mgongo na kiuno, kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa hamu ya kula, kutokwa na uchafu wa majimaji uliopauka wenye rangi ya kahawia au wenye damu na kuvimba mguu mmoja.
Ili kuwanusuru watoto kukumbwa na tatizo hilo, aliwataka wazazi kuwapeleka watoto kwenye vituo vya kutolea chanjo kupata kinga kwa kuwa kinga ni bora zaidi kuliko tiba.
Alisema saratani ya mlango wa kizazi na kansa ya ziwa zimekuwa zikisababisha vifo vingi kwa wanawake hasa kwa wale walioanza kujamiana katika umri mdogo.
Dk. Mutahyabarwa alisema imekuwa rahisi kuambukizwa maradhi hayo kutokana na sehemu za mwili ambazo bado hazijakomaa kufanya tendo hilo la ndoa.
Mganga mkuu huyo alisema chanjo hiyo ambayo ni endelevu inatekelezwa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwamba serikali imejipanga kuhakikisha ugonjwa huo unabakia kuwa historia kama ilivyo kwa ugonjwa wa pepopunda ambao uliua watu wengi kwenye miaka ya 1970 kabla ya kugundulika kwa chanjo.
Aidha, aliwaasa kinamama kuachana na matumizi ya sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi ambavyo ni miongoni mwa visababishi vya maambukizi ya saratani hiyo kupitia virusi vya papilloma.
Alisema katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa, chanjo hiyo itakuwa endelevu na aliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa watoto wenye umri wa miaka 14, watahamia kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka tisa hadi 14.

No comments:
Post a Comment