Muongozaji wa Mahiri wa video za muziki wa Injili kutoka jijini Nairobi Kenya anayefahamika kwa jina la Director Bakari Ousman kutoka lebo ya Crosslife Movement anatarajiwa kuja Tanzania mwezi wa tano mwaka 2018, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza na maalumu kwa ajili ya kupanua mipaka ya kazi yake nchini Tanzania.
Akizungumza na gospomedia.com Director Bakari Ousman alisema kuwa kusudi la ziara hiyo ni kutafuta na kupata waimbaji wa nyimbo za injili ambao wana nyimbo nzuri lakini hawana video, Ambapo amesema atawafanyia video hizo bila malipo kwa waimbaji wawili ambao watakachaguliwa na lebo ya Crosslife Movement ikisaidiana na kampuni ya Gospo Media.
“Ziara hii pia itawahusu waimbaji wenye uhitaji wa video zenye ubora wakiwa na uwezo mdogo kifedha ilimradi tu nyimbo zao ni nzuri mimi nitawasaidia. Baadae nitawaingiza waimbaji wawili katika menejimenti ya record label yetu ya Crosslife Movement ambayo tunatarajia kuizindua rasmi mwishoni mwa mwaka huu kama Mungu akitupa nguvu na kibali. Waimbaji hao watapata fursa ya kurekodi nyimbo na video katika studio zetu tukishirikiana na producers(watayaarishaji) kutoka Tanzania na huku Kenya ili kupata kazi bora zaidi.” – Alisema Bakari Ousman
Director Bakari Ousman ni moja kati ya waongozaji mahiri na wabunifu wanaofanya vizuri kwasasa katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Kenya, Ambapo mpaka sasa tayari ameshafanya kazi nyingi ambazo kwa hakika zimemtambulisha vyema katika uliemwengu wa muziki wa Injili kutokea Kenya, Na moja kati ya video ambazo amefanya na kufanya vizuri ni pamoja na Umenibeba – Godwill Babette, Waweza – Marion Shako na Wewe ni Mungu – Neema K
Nakuja kuwasaidia waimbaji Tanzania – Director Bakari Ousman, Crosslife Movement.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment