Michuano ya klabu bingwa barani
Ulayani, hatua ya robo fainali inaendelea usiku wa kuamkia leo. Michezo
miwili imepigwa ambapo Barcelona wakiwa nyumbani dhidi ya As Roma
wamepata ushindi wa mabao 4-1.
Mabao ya Barcelona katika mchezo
huo, yamefungwa na wachezaji De Rossi ,Kostas Manolas ambao walijifunga
wenyewe.Goli la tatu limefungwa na Gelard Pique huku bao la nne
likipachikwa na Luis Suarez, bao la kufutia machozi la As Roma
likifungwa na Edin Dzeko.
Katika mchezo mwingine Liverpool wao
wamewachapa bila huruma vinara wa ligi kuu ya England Manchester city
bao 3-0, Magoli ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah, Oxlade
Chamberlin pamoja na Sadio Mane.
Robo fainali nyingine ya pili
itafanyika tarehe 10 mwezi April kwa michezo miwili,As Roma itacheza
dhidi ya Barcelona na Manchester City itachuana na Juventus, na Aprili
11 Bayen Munich itacheza na Sevilla huku Real Madrid ikicheza na
Juventus.
No comments:
Post a Comment