Muimbaji wa nyimbo za Injili jijini Dar es salaam Martha Mwaipaja
amefunguka na kusema kuwa katika dunia ya sasa watu wamekuwa wakifanya
sana dhambi na kuzini ili hali wanatambua kuwa kufanya hivyo ni makosa
lakini wamekuwa wakimsingizia shetani.
Martha Mwaipaja amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI
kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV na kudaikwamba yeye
amekuwa hawaelewi watu ambao wanafanya zinaa halafu wanasema wamepitiwa
na shetani na kudai kuwa hilo jambo si kweli kwani wao wanapofanya hivyo
wanakuwa wanatambua na kupanga kufanya tendo hilo ndiyo maana hawawezi
kulifanya wakiwa sebuleni.
No comments:
Post a Comment