Godfrey Saulo na wimbo wake mpya uitwao Niwe Mtoto



 
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Tanzania  aliyewahi kufanya vizuri na wimbo wa Baraka ni  Sumaku Godfrey Saulo achia wimbo mpya uitwao Niwe Mtoto.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Saulo amesema kuwa alikuwa kimya  baada ya Baraka ni Sumaku ni kwa sababu alikuwa anataka kutoa kazi nzuri zaidi tofauti.

Saulo amesema kuwa  Sababu nyingine ambayo imefanya aweze kuchelewa kuachia wimbo mwingine ni kutaka kutoa nyimbo ambayo ni tofauti na nyimbo zake za awali kama vile Baraka ni sumaku sio kila kingaacho ni Dhamu, Wanafanana na sanamu nayingine nyingi.

Hata hivyo Saulo amesema wimbo wake huo wa Niwe Mtoto mpaka sasa unapatikana kwenye Mtandao na kuhusu video ipo njiani muda sio mrefu itakuwa tayari.

No comments:

Post a Comment