Wakristo
wametakiwa kusheherekea sikuku ya Pasaka kwa
amani na utulivu na kujitenga na
uovu.
Hayo yamesemwa na
askofu wa kanisa la FPCT Tanzania David Batenzi wakati akihubiri katika ibada
ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa la
FPCT Kimahani lililopo Arusha Mjini.
Amesema kuwa
sikuku ya Pasaka ni kiini cha ukristo
hivyo ni vema wakristo wakasheherekea kwa kumaanisha kiroho na Kimwili kwani
ukristo wenye nguvu msingi wake ni msalaba.
Askofu Batenzi
amewataka wakristo kumuamini yesu badala
ya kuamini miungu wengine kwa minajili
ya kufanikisha jambo kwani kwa kufanya hivyo ni kumkufuru mungu.
Hata hivyo Askofu
Batenzi amehitisha mkutano wa Pasaka mkoani
Arusha na anatarajia kurudi Daresalaama kwaajili ya Shughuli za Kikanisa.
No comments:
Post a Comment