Askofu mkuu wa kanisa la FPCT Tanzania amewasili mkoani Arusha kwaajili ya Mikutano ya Pasaka ambayo itakuwa ikifanyika katika kanisa la FPCT Kimahama .
Akizungumza na Blog hii Makamo askofu mkuu wa mkoa wa Arusha
Mchungaji Muna amesema Akofu Batenzi atahudumia mikutano yote ya Pasaka ambayo
itakuwa inafanyika katika kanisa la
kimahama.
Aidha kwa upande wake Askofu Batenzi akielezea ripoti ya mkutano wa umoja wa
makanisa duniani ulio fanyika Ngurudoto mwanzoni mwa mwezi wa tatu Mkoani Arusha baada ya kuwasili na ndege akitokea Daresalaam amesema ni vema makanisa yakawa na umoja katika kueneza injili kwa
watu wote.
Askofu Batenzi
ataongoza mikutano yote ya Pasaka
na baada ya pasaka kupita atarejea mkoani Daresalaam kwaajili ya
shughuli mbalimbali za kikanisa.
No comments:
Post a Comment