Mwanafunzi wa kidato cha pili mkoani Mtwara, Salma Abdalah aliyekuwa akiishi Mbawala Chini, amefariki dunia kwa kujinyonga, baada ya kukutwa na simu ambayo alipewa na mpenzi wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara
Lucas Mkondya, amesema tukio hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii baada
ya wazazi wa binti huyo kuamua kumfukuza nyumbani na kumtaka kwenda
kuishi kwa bibi yake kutokana na utovu wa nidhamu, na ndipo akaamua
kujitoa uhai wake.
Kamanda Mkondya ameeleza kuwa wazazi wake waligundua kuwa binti yao
alikuwa akimiliki simu ambayo hawajamnunulia na walipomuuliza hakuwa na
jibu sahihi, ndipo baba yake ambaye ni baba wa kufikia aliamua kumfukuza
nyumbani kutokana na kuchoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamu, na
kuelekea sokoni kwenye biashara zake kumtafutia nauli, huku mama yake
akielekea shambani kwenye shughuli zake za kilimo,
Taarifa zaidi kutoka kwa mashuhuda wa tukio wamesema binti huyo
alipojinyonga aliacha ujumbe uliosema kwamba "Nampenda sana Daudi,
siwezi kukaa naye mbali najua hili ni kosa kwangu lakini nawaomba wazazi
wangu mumpende sana Daudi maana akiwa kwenye matatizo, mimi sitajisikia
vizuri"
No comments:
Post a Comment