Waziri wa Nchi Ofisi ya Rasi Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo mapema kesho Tar.02/01/2018 atafanya
ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Arusha Dc iliyopo Mkoani Arusha.
Akizungumzia Ziara hiyo Mhe. Jafo amesema ni
ziara ya kawaida ya kikazi akiwa katika Halmashauri hiyo ataonana na
Watumishi wa Halmashauri ili kuweza kuskiliza kero zao na pia
atatembelea Shule ya Sekondari Ilboru kukagua Ukarabati wa shule hiyo
kongwe unaoendelea.
Zaidi ya hapo Waziri Jafo amesema atatembelea,
kukagua na kuweka Jiwe la Msingi katika kituo cha Afya ya Nduruma kisha
atazungumza na wananchi wa eneo hilo katika Mkutano wa hadhara
utakaofanyika katika viwanja vya kituo cha Afya Nduruma.
Hii ni ziara ya kwanza ya kikazi ya Waziri Jafo
kwa Mwaka huu wa 2018 na baada ya halmashauri hii ataendelea na ziara
yake katika Halmashauri za Korogwe, Kisarawe,Dar ea Salaam, Kilolo na
atafika katika Mikoa ya Mbeya, Lindi na Mtwara.
Kasi ni ile ile kwa mwaka mpya wa 2018, Tamisemi ya Wananchi.
No comments:
Post a Comment