Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imewahukumu kifungo cha maisha jela
washitakiwa watatu baada ya kuwatia hatiani kwa kuchoma Kanisa la EAGT
mwaka 2015.
Hukumu imetolewa leo Jumanne Januari 2,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Charles Oisso baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa
mashtaka kuwa washtakiwa walitenda makosa ya kula njama na kuchoma
kanisa hilo eneo la Omukibeta, Manispaa ya Bukoba.
Waliohukumiwa ni Rashid Athuman, Ngesela Ismail na Ally Hassan ambao
walidaiwa kutenda makosa hayo kutokana na chuki dhidi ya dini nyingine
jambo ambalo Mahakama imesema lingesababisha uvunjifu wa amani na
usalama.
Washtakiwa tayari wako gerezani wakitumikia kifungo cha maisha baada ya
kutiwa hatiani katika shauri lingine namba 178 la mwaka 2015 ambalo pia
linahusu kuchoma makanisa katika maeneo tofauti mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment