Tanzania inakusudia kutanua wigo katika kukuza sekta ya
utalii hasa utalii wa asili ambao kwa miaka umekuwa ukiifanya
Tanzania kushika nafasi za juu duniani,jambo linalotarajiwa ongeza
idadi ya watalii na kuongeza pato la taifa.
Akizungumza na kituo hichi kaimu mkurugenzi wa taasisi
ya wanyama pori TAWA,jemsi Wakibara amesema utanuzi huo unaenda sambamba na
utunzaji wa mapori ya akiba ambayo ndio kiini cha ustawi wa hifadhi hapa
nchini.
Licha ya jitihada hizo zinazofanywa na wadau mbalimbali bado
jitihada za makusudi zinahitajika katika kupambana na ujangili ambao kwa
kipindi kirefu umekuwa ukitikisa sekta hiyo kama anavyo eleza Alex Choyo meneja
wa pori la Swagwaswaga.
Emanuel mashana meneja wa pori la Mkongonere ambae
anaeleza umuhimu wa maporo ya akiba kwa ustawi wa hifadhi za tanzania
huku akitolea mfano hifadhi ya Tarangire.
Mapori ya akiba hapa nchini tangu kuanzishwa kwake yameelezwa
kuwa na mchango mkubwa katika sekta ya utalii licha ya kukambiliwa na
changamoto mbalimbali katika uendeshaji wake.
No comments:
Post a Comment