Leo January 5, 2017 Mfanyabiashara James
Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi
wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai
awali kuwa atawataja.
Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad
Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba
iahirishwe hadi tarehe nyingine.
“Mwizi ni Standard Chartered Tanzania
Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali
hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea TAKUKURU washiriki wengine wa
fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi
mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” – James Rugemarila
Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio
wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai
Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha
taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.
Tofauti na hayo Rugemarila pia ameiomba
mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini India kwa sababu
anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku mshtakiwa
mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi aliiambia
Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.
Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema
afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka
upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha
kesi hiyo hadi January 19,2018.
No comments:
Post a Comment