Miezi miwili baada ya kuhifadhi kiti
chaka cha Urais, Uhuru Kenyatta ameanza kuunda baraza lake jipya kwa
kuwateua tena mawaziri sita wa zamani.
Kinachoshangaza wadadisi wa maswala ya kisiasa ni kutangazwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya, Bw KeriakoTobiko kuwa waziri. Hii ni mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kutangaza kwamba amekubali maombi ya Bwana Tobiko ya kujiuzulu kama Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya.
Waliohifadhiwa katika baraza hilo jipya ni Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiangi, Waziri wa fedha Bwana Henry Rotich, Waziri wa Utalii Najib Balala, na Bwana Joseph Mucheru akihifadhi wadhifa wake wa Waziri wa Teknolojia na Habari.
Waziri wa Mawasiliano amesalia kuwa Bwana James Macharia na Waziri wa Kawi ni Bwana Charles Keter.
Wanasiasa walipoendekezwa na rais kushikilia wadhifa wa uwaziri ni aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Turkana ,John Munyes na aliyekuwa Govana wa Marsabit , huko Mashariki mwa Kenya Bwana Ukur Yatani ,
Kiongozi huyo wa Kenya anayehudumu kwa kipindi chake cha pili na cha mwisho kama rais amesema bado yuko katika harakati ya kubuni baraza lake kamili .
Katiba ya Kenya inasema kwamba baraza la mawziri sharti liwe na mawaziri kati ya 14 na wasizidi 22.
Rais Uhuru Kenyatta aliingia madarakani kuwa awamu wake pili baada ya kutangazwa mshindi wa urais baada ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya mwezi Oktoba mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment